Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 1,176 vyathibitishwa Ujerumani

Idadi ya kesi za maambukizi ya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 253,474, baada ya kesi mpya 1,176 kuthibitishwa, idadi ambayo ni kumbwa ikilinganishwa na siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa na kituo cha kudhibiti na kuzuia maradhi ya kuambukia Robert Koch (RKI).

Kulingana na RKI, vifo vingine tisa vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,338 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.
Kulingana na RKI, vifo vingine tisa vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,338 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani. AFP/Ronny Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na RKI, vifo vingine tisa vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,338 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Maambukizi duniani kote hadi sasa ni zaidi ya watu milioni 27, na zaidi ya watu 890,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

Wakati huo huo majaribio ya mwisho ya chanjo ya virusi vya Corona, yaliyokuwa yanafanywa na kampuni ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford yamesitishwa kwa muda baada ya mtu aliyekuwa anajaribiwa chanjo hiyo kuumwa.

"Hii ni hatua ya kawaida ambayo inapaswa kutokea wakati kuna uwezekano wa ugonjwa ambao haufahamiki katika moja kati ya majaribio, wakati unachunguzwa, na kuhakikisha tunaendelea uhalali wa majaribio, " amesema msemaji wa kampuni ya madawa inayotengeneza chanjo hiyo AstraZeneca.

Kwa mujibu wa Stat News, mgonjwa huyo aliyejitolea kufanyiwa majaribio ya chanjo ana uwezekano wa kushiriki katika awamu ya 2 na ya tatu ya majaribio nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.