Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Ujerumani yaonya raia wake kusafiri katika baadhi ya maeneo ya Uhispania

Taasisi inayodhibiti magonjwa nchini Ujerumani inasema inahofia ongezeko la maambukizi ya Corona nchini humo, huku ikionya raia wake dhidi ya kusafiri katika baadhi ya majimbo nchini Uhispania.

Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi.
Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa taasisi hiyo Lothar Wieler, amesema kuwa maambukizi hayo ambayo yalionekana kupungua sasa yameanza kuongezeka tena, suala ambalo amesema linazua wasiwasi.

Ujerumani ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Mbili, imeonekana ikipiga hatua kubwa kuhusu namna inavyodhibiti maambukizi hayo katika jamii, ikilinganishwa na nchi jirani, lakini kasi ya maambukizi katika siku za hivi karibuni, imezua wasiwasi.

Raia wa nchi hiyo sasa wametakiwa kuheshimu kanuni za Wizara ya Afya na kuhakikisha kuwa wanavalia barakoa kila wakati wanapokuwa nyumbani na maeneo mengine ya umma.

Hili ni onyo linalokuja wakati huu dunia ikishuhudia ongzeko la virusi vya Corona, huku Wizara ya Mambo ya Nje nchini Ujerumani ikiwataka raia wake kutoenda katika majimbo matatu Kaskazini mwa Uhispania, yanayoaminiwa kuendelea kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.

Ujerumani imekuwa ikisifiwa kwa kutoa huduma ya haraka kwa watu walioambukizwa katika taifa hilo, ambalo limeshuhudia vifo vya watu zaidi ya Elfu Tisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.