Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Zaidi ya kesi 194,000 zathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya kesi za maambukizi ya virisi vya Corona zilizothibitishwa nchini Ujerumani imepanda hadi 194,259, baada ya kesi mpya 498 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita, kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Robert Koch (RKI).

Vifo vipya 12 vimerekodiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya vifo kufikia 8,973 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.
Vifo vipya 12 vimerekodiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya vifo kufikia 8,973 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya 12 vimerekodiwa, kulingana na RKI, na kufanya jumla ya vifo kufikia 8,973 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani, WHO, limetahadharisha kuwa hali ya maambukizi ya virusi vay Corona itakua mbaya zaidi siku za usoni, ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.

Zaidi ya watu Milioni 10 wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi duniani tangu virusi hivyo vilipojitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka uliopita.

Hata hivyo idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 500,000.

Marekani na Brazili zinaongoza kwa maambukizi zaidi, na vifo zaidi duniani.

Mkuu wa shirika la Afya Dunia (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amezitaka serikali kufuata mifano ya Ujerumani, Korea Kusini na Japan, ambazo zimekuwa zikichukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kutumia sera ikiwemo vipimo na ufuatiliaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.