Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Ujerumani kuanza kulegeza masharti ya usafiri katika nchi za EU Juni 16

Ujerumani inatarajia kuanza kulegeza vizuizi vya kusafiri katika nchi za Umoja Ulaya, Uswizi, Iceland, Norway, Uingereza na Liechtenstein kuanzia Juni 15 ikiwa kutakuwa na maendeleo katika vita dhidi ya janga Corona katika nchi hizo, vyanzo vya serikali vimebaini.

Kufikia sasa Ujerumani inarekodi visa 184,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 213 kuthibitishwa ndani ya kipndi cha saa 24.
Kufikia sasa Ujerumani inarekodi visa 184,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 213 kuthibitishwa ndani ya kipndi cha saa 24. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kuondolewa kwa masharti haya yaliyowekwa katikati mwa mwezi Machi ili kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona pia kutaendana na masharti juu ya kufunguliwa kwa mipaka ya nchi husika kwa wasafiri kutoka Ujerumani, vyanzo hiyo vimeongeza.

Kufikia sasa Ujerumani inarekodi visa 184,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 213 kuthibitishwa ndani ya kipndi cha saa 24.

Wagonjwa 166,000 wamepona ugonjwa wa Covid-19, ugonjwa ambao umesababisha vifo vya jumla ya watu 8,674 baada ya ifo vipya 11 kuthibitishwa ndani ya kipindi cha saa 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.