Pata taarifa kuu
EU-CORONA-AFYA

Virusi: Umoja wa Ulaya wafungua tena sehemu ya mipaka yake, WHO yatahadharisha

Umoja wa Ulaya, ambapo janga la Covid-19 linapungua kwa kasi, limefungua tena mipaka yake kwa nchi 15, lakini shirika la Afya Dunia (WHO) limeonya kwamba janga hilo halipo karibu kumalizika.

Baada ya siku kadhaa za mazungumzo, nchi za Umoja wa Ulaya zimeamua leo Jumanne kufungua tena mipaka yao kuanzia Julai 1 kwa raia kutoka nchi 15 ambazo hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha.
Baada ya siku kadhaa za mazungumzo, nchi za Umoja wa Ulaya zimeamua leo Jumanne kufungua tena mipaka yao kuanzia Julai 1 kwa raia kutoka nchi 15 ambazo hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha. Kenzo TRIBOUILLARD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.

Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema juma lijalo WHO, itapeleka ujumbe wake China, ambako ugonjwa huo ulizuka miezi sita iliyopita kwa lengo la kutafuta kiini chake.

Baada ya siku kadhaa za mazungumzo, nchi za Umoja wa Ulaya zimeamua leo Jumanne kufungua tena mipaka yao kuanzia Julai 1 kwa raia kutoka nchi 15 ambazo hali yao ya ugonjwa huchukuliwa kuwa ya kuridhisha, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

Covid-19 bado inaathiri kwa kasi katika maeneo ya Marekani, ambako kumerekodiwa vifo zaidi ya 125,000 na maambukizi milioni 2.5. Makadirio hayo yanaweza kufikia robo ya maambukizi yote ulimwenguni.

Baraza la Umoja wa Ulaya limesema hivi leo kwamba nchi hizo salama ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay.

Kundi hilo la mataifa 27 linatazamiwa kutoa muongozo unaolegeza au kuruhusu safari za matembezi ama kibiashara kuanzia kesho Jumatano kwa mataifa hayo.

Urusi na Brazil, kama ilivyo Marekani, hazikukidhi vigezo vya mataifa yaliyo salama kutokana na janga la Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.