Pata taarifa kuu
EU-CORONA-AFYA

Coronavirus: EU yaahirisha uamuzi wake kuhusu mipaka yake

Wajumbe wa Umoja wa Ulaya wameshindwa kupitisha orodha ya mwisho ya nchi za ulimwengu wa tatu zinazoonekana salama ambazo raia wao wanaweza kusafiri kwenda katika nchi wanachama wa umoja huo kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Makao makuu ay Umoja wa Ulaya, Brussels.
Makao makuu ay Umoja wa Ulaya, Brussels. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani, Brazili na Urusi hazipaswi kujumuishwa kwenye orodha hii kwa sababu zinaendelea kurekodi maambukizi zaidi ya virusi vya Corona.

Mabalozi kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya wamekutana kujaribu kuweka vigezo kuhakikisha kwamba kuanzia Jumatano raia wa kigeni kutoka nchi za ulimwengu wa tatu wanaingia katika nchi hizo wanachama wa Umoja wa Ulaya bila kuwekwa karantini.

Orodha ya nchi 10 hadi 20 zimewasilishwa, lakini mabalozi wengi wamesema wanahitaji kushauriana na serikali zao, wanadiplomasia wamebaini.

Orodha hiyo haikujumuisha Marekani, Brazili na Urusi, kulingana na mwanadiplomasia aliyeshiriki mkutano huo.

Kulingana na maafisa wawili wa Marekani abiria kutoka Marekani wataruhusiwa kusafiri ikiwa watatimiza masharti kadhaa ikiwemo kupita katika vituo vya ukaguzi wa joto la mwili.

Serikali za nchi 27 wanachama wa EU zinatarajiwa kutoa majibu ya kwanza kuanzia leo Jumamosi jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.