Pata taarifa kuu
UINGEREZA-CORONA-AFYA

Serikali ya Uingereza yakumbwa na mvutano kuhusu mshauri wa Johnson

Mjumbe katika serikali ya Uingereza amejiuzulu Jumanne wiki hii kufuatia utata kuhusu Dominic Cummings, mshauri wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ambaye alivunja marufuku ya kutotembea wakati nchi hiyo ilikuwa ko chini ya marufuku ya kutotembea.

Dominic Cummings, mshauri wa Waziri Mkuu Boris Johnson, aliliponea kuangushwa kwa serikalini licha ya mvutano. Hapa, anaondoka nyumbani kwake muda mfupi kabla, Mei 24, 2020.
Dominic Cummings, mshauri wa Waziri Mkuu Boris Johnson, aliliponea kuangushwa kwa serikalini licha ya mvutano. Hapa, anaondoka nyumbani kwake muda mfupi kabla, Mei 24, 2020. REUTERS/Simon Dawson
Matangazo ya kibiashara

Maelezo ya Dominic Cummings hayakuweza kuzima mvutano huo.

Tayari Dominic Cummings amekosolewa kwa usimamizi wake wa kudhibiti janga la Covid-19 na mpango wake wa kuanza kulegeza baadhi ya hatua za kudhibiti ugonjwa aw Corona.

Hata hivyo Waziri Mkuu Boris Johnson amejaribu kuja juu na kumtetea mshauri wake.

"Wakazi wa eneo langu hawakuweza kusema kwaheri kwa wapendwa wao, familia hazikuweza kuomboleza kwa pamoja, watu hawakuweza kutembelea wapendwa wao wagonjwa kwa sababu walifuata maagizo ya serikali. "amesema, Katibu dola wa Jimbo la Scotland, Douglas Ross, kwenye Twitter.

"Siwezi kuwaambia kwa ukweli kwamba wote walikosea na kwamba mshauri wa serikali alikuwa sahihi," ameongeza.

Katika mkutano wa kipekee na waandishi wa habari, Dominic Cummings hakuomba msamaha au kujutia kitendo chake lakini alihakikisha kuwa kitendo chake alikifanya kwa njia ya "kisheria na busara" kwa kutembea kilomita 400 licha ya marufuku ya kutotembea iliyokuwa imewekwa kwa wananchi wa Uingereza.

Kwa kuhofia kuambukizwa virusi vya Covid-19, anasema alikwenda na mke wake na mtoto wa miaka minne nyumbani kwa wazazi wake huko Durham, Kaskazini Mashariki mwa Uingereza, kwa sababu alikuwa anatafuta suluhisho la nani atabaki na mwanaye.

Safari ya pili imekosolewa hasa wakati alipotembelea jumba la kale la Barnard, kama kilomita arobaini kutoka nyumbani kwa wazazi wake, siku ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mkewe. Mshauri huyo alihakikisha kwamba kitendo hicho cha kusafari kwa gari kungelimuwezesha achunguze kuwa anaweza kuendesha kwa usalama kwa sababu macho yake yameathiriwa na virusi.

Licha ya serikali kujaribu kumtetea mshauri wa waziri mkuu, hali sio nzuri, ikiwa ni pamoja na katika kambi za Conservatives ambapo karibu wabunge kumi na tano wanamtaka ajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.