Pata taarifa kuu
UINGEREZA-JOHNSON-CORONA-AFYA

Uingereza kurejelea shughuli zake za kawaida mwezi Juni

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kuwa, nchi hiyo itaanza kurejelea shughuli zake taratibu kuanzia tarehe 1 mwezi Juni. Hii ni "sehemu ya kwanza" ya "mpango" wa kuondo amarufuku ya kutotoka nje uliowekwa kudhibiti maambukizi ya Corona.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutoa maelezo zaidi mbele ya Bunge kuhusu kurejesha hali ya kawada nchini humo Jumatatu wiki hii
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutoa maelezo zaidi mbele ya Bunge kuhusu kurejesha hali ya kawada nchini humo Jumatatu wiki hii PRU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Johnson amesema kufuguliwa kwa shule, maduka na maeneo ya umaa itategemea pakubwa na hali ya maambukizi ya Corona nchini humo.

Siku ya Jumapili katika hotuba Boris Johnson aliyoyangaza kwa njia ya televisheni kwa taifa, Bwana Johnson ''alitangaza mpango wa hali'', wa kufungua shughuli za kijamii, kuwaruhusu raia wa Uingereza, kufanya shughuli zao nje ya makazi yao kwa muda zaidi kuanzia Jumatano.

Uingereza imeshuhudia vifo vya watu 32, 0000 vilivyotokana na mamabukizi ya Corona, huku maelfu wakiambukizwa, ikiwa nchi ya pili baada ya Marekani duniani kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.

Waziri Mkuu wa Uingereza anatarajiwa kutoa maelezo zaidi mbele ya Bunge kuhusu kurejesha hali ya kawada nchini humo Jumatatu wiki hii, huku taarifa zaidi kuhusu mfumo wa utambuzi wa Covid-19 , matumizi ya barakoa, na kurejea kwa soka ya kulipwa zikitaraji wa kutolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.