Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAANDAMANO-USAFIRI

Mgomo mkubwa wazorotesha shughuli katika sekta mbalimbali Ufaransa

Ufaransa imekumbwa na mgomo mkubwa wa wafanya kazi ambao hayajawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi nchini humo, mgomo ambao umeathiri sekta ya usafiri wa umma, huku shule zikifungwa.

Makumi ya maelfu ya watu walimiminika mitaani Alhamisi, Desemba 5 katika miji mbalimbali ya Ufaransa.
Makumi ya maelfu ya watu walimiminika mitaani Alhamisi, Desemba 5 katika miji mbalimbali ya Ufaransa. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa polisi, mawakili, wafanyakazi wa hospitali na viwanja vya ndege wameungana na wafanyakazi wa mashuleni na sekta ya usafiri wa umma katika mgomo wa kitaifa ambao huenda ukajumuisha mamilioni ya watu.

Maafisa wa polisi 6,000 wamepelekwa katika maeneo mbalimbali kushika doria, kukabili kile kinachotizamiwa kuwa yatakuwa maandamano makubwa katika mji mkuu Paris, huku vituo vingi vya treni vikiwa vimefungwa.

Mamlaka inayosimamia usafiri wa treni SNCF imesema safari za takriban treni 9 kati ya 10 za mwendo kasi zimesitishwa. Aidha asilimia 30 ya safari za ndege za ndani nchini humo pia zimesitishwa kufuatia mgomo huo.

Maandamano kadhaa yamefanyika katika miji mbalimbali ya Ufaransa dhidi ya muswada wa serikali kuhusu mageuzi ya hazina ya uzeeni.

Wafanyakazi wameghabishwa na mpango wa kuwalazimisha kustaafu kuchelewa ama malipo yao ya uzeeni yapunguzwe.

Waziri wa uchukuzi amesema atakutana na vyama vya wafanyakazi kujaribu kuondoa wasiwasi.

Maandamano hayo makubwa yaliidhinishwa na chama cha wafanyakazi ambacho hakijafurahishwa na mipango ya rais Macron ya kutaka kuanzisha mfumo wa malipo ya uzeeni ambapo kila siku moja iliyofanyiwa kazi inapata alama kwa ajili ya mapato ya pensheni ya siku za usoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.