Pata taarifa kuu
ITALIA-EU-UCHGUZI

David Sassoli achaguliwa rais wa Bunge la Ulaya

David Sassoli mwenye umri wa miaka 63, na mwandishi wa habari wa zamani wa televisheni nchini Italia, na mbunge wa Ulaya kutoka mrengo wa kushoto tangu mwaka 2009, amechaguliwa Jumatano wiki hii kuwa rais wa Bunge la Ulaya kwa muhula wa miaka miwili na nusu.

David Sassoli rais mpya wa Bunge la Ulaya, Jumatano Julai 3.
David Sassoli rais mpya wa Bunge la Ulaya, Jumatano Julai 3. REUTERS/Vincent Kessler
Matangazo ya kibiashara

Siku moja maada ya maelewano yaliyofikiwa na viongozi wa nchini 28 za Umoja wa Ulaya mjini Brussels ili kujaza nafasi muhimu za taasisi hiyo, David Sassoli, raia wa Italia amechaguliwa kuwa urais wa Bunge la Ulaya.

Amemrithi Antonio Tajani, aliye karibu na Silvio Berlusconi kutoka chama cha EPP cha mrengo wa kulia.

Italia, inashikilia nafasi tatu muhimu.

David Sassoli amechaguliwa kwa kura 345. Amepata wingi wa kura zilizopigwa kwa siri katika duru ya pili mjini Strasbourg.

David Sassoli amekuwa akishindana na mbunge, ambaye ni mwanamazingira kutoka Ujerumani Ska Keller, ambaye amepata kura 119 katika duru ya pili, Sira Rego (43), raia wa Uhispania kutoka chama cha mrengo wa kushoto na Jan Zahradil, raia wa Ukraine (amepata kura 160).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.