Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Dominic Raab, ateuliwa kuwa waziri mpya wa masuala ya Uingereza kujitoa katika EU

Dominic Raab, mpaka sasa Waziri wa Nyumba, ameteuliwa kuchukua nafasi ya waziri anayehusika na masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya. Uteuzi ambao umefanyika Jumatatu hii, Julai 9.

Dominic Raab waziri mpya anayehusika na masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Julai 9, 2018.
Dominic Raab waziri mpya anayehusika na masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Julai 9, 2018. REUTERS/Henry Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amechukua hatua ya haraka kufuatia kujiuzulu kwa David Davis kwenye nafasi hiyo. Theresa May amemteua Dominic Raab kwenye nafasi ya David Davis ambaye hakuwa na haja ya kudumisha uhusiano wa kibiashara wa karibu na Umoja wa Ulaya.

Dominic Raab ana uzoefu mdogo wa kwenye wizara hiyo. Raab ambaye ana umri wa miaka 44, mpaka sasa ameteuliwa kwenye nafasi mbili tu, kwenye Wizara ya Sheria na kwenye Wizara ya Nyumba

Kwa upande wa Theresa Mei sasa, anasema kipaumbele ni kuzima moto haraka iwezekanavyo ili kuepuka hali ya sintofahamu kuzuka kati ya "wanaharakati wanaotaka Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya".

Waziri Mkuu anatarajia kuhutubia bunge Jumatatu hii mchana ili kuwakilisha rasimu hiyo mpya, na baadaye jioni, atakutana na watu kutoka kambi yake ya Conservative ili kujaribu "kutoa" pendekezo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.