Raia wa Italia wasubiri matokeo ya Uchaguzi wa wabunge
Matokeo ya awali kuhusu Uchaguzi wa Wabunge nchini Italia, yanaonesha kuwa hakuna chama kitachopata idadi kubwa ya viti vinavyohitajika ili kuunda serikali pekee yake.
Imechapishwa:
Hata hivyo, hadi sasa muungano wa siasa unaoegemea mrengo wa kulia, unaongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi unatarajiwa kushinda.
Hata hivyo, ushindi huo unatarajiwa kuwa kati ya wabunge 225 au 265 kinyume na wabunge 316 kama inavyohitajika ili kuunda serikali.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kufahamika baadaye siku ya Jumatatu.
Chama kitakachounda serikali, kitakuwa na kazi kubwa ya kuimarisha uchumi, kuunda nafasi za kazi na kupambana na wimbi la wakimbizi wanaokimbilia nchi hiyo.