Pata taarifa kuu
MAREKANI-UBELGIJI-NATO

Trump kuhudhuria mkutano wa NATO

Rais wa Marekani Donald Trump aliwasili Jumatano 24 Mei katika mji wa Brussels kama sehemu ya ziara yake ya kwanza ya kimataifa na anatazamiwa kuondka Alhamisi hii jioni.

Malkia Mathilde na Mfalme Philip pamoja na Waziri Mkuu Charles Michel mjini Brussels wakiwa pamoja na Melania na Donald Trump Mei 24, 2017.
Malkia Mathilde na Mfalme Philip pamoja na Waziri Mkuu Charles Michel mjini Brussels wakiwa pamoja na Melania na Donald Trump Mei 24, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana na mfalme wa Ubelgiji na waziri wake mkuu siku ya Jumatano, rais Trump anaendelea na ratiba yake siku ya Alhamisi asubuhi na viongozi wa Umoja wa Ulaya kabla ya chakula cha mchana pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kushiriki katika mkutano wa kwanza wa muungano wa nchi za kujihami za Magharibi (Nato).

Rais Donald Trump anatazamiwa kuondoka ncini Ubelgiji Alhamisi hii jioni. Tangu kuwasili kwa Donald Trump katika uwanja wa ndege wa Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji umewekwa chini ya ulinzi mkali. Mashambulizi katika mji wa Manchester yalikumbusha mashambulizi mawili yaliotokea kwa wakati mmoja nchini Ubelgiji katika uwanja wa ndege na katika eneo ambako kunapatikana makao makuu ya Umoja wa Ulaya ambapo Donald Trump anazuru wakati wa ziara hii mjini Brussels.

Wakati wa ziara hii ya zaidi ya masaa thelathini ya Donald Trump katika mji wa Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji umewekwa chini ya ulinzi mkali hata kama Waziri wa Mambo ya Ndani haonyesha umuhimu wa kutaja kiwango cha tishio ambacho kinabaki kwenye kiwango cha juu kabisa. Usalama umeimarishwa mjini Brussels.

Mbali na askari wanaopiga doria tangu mashambulizi yaliyoikumba Ubelgiji mwaka uliopita, zaidi ya polisi elfu nne wa nchi hiyo wametumwa katika maeneo mbalimbali na wamepewa uwezo wa kutoshaikiwa ni pamoja na, helikopta.

Maeneo ya mji wa Brussels yamezingirwa tangu siku ya Jumatano alasiri na barabara zimefungwa na vizuizi hadi kuondoka kwa Donald Trump.

Maandamano dhidi ya uwepo wake mjini Brussels yamepigwa marufuku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.