Pata taarifa kuu
USWISI-URAIA-WAHAMIAJI

Kura ya ndiyo yapigwa kwa uraia wa wajukuu wa wahamiaji

Jumapili hii Februari 12 kura ya maoni imepigwa kwa idadi kubwa nchini Uswisi, kwa minajili ya kurahisisha mchakato wa uraia wa wajukuu wa wahamiaji, licha ya kampeni za mrengo wa kulia zilizoendeshwa kwa hotuba za kupambana na Waislamu, kwa mujibu wa matokeo ya mwisho.

Polisi katika Kituo cha Salez, nchini Uswisi, ambako shambulizi lililowajeruhi watu sita katika treni.
Polisi katika Kituo cha Salez, nchini Uswisi, ambako shambulizi lililowajeruhi watu sita katika treni. AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya 60.4% ya wananchi wa Uswisi wameonga mkono pendekezo la serikali ya Uswisi. Kwa kukubaliwa, agizo hili la serikali linapaswa kupata wingi wa majimbo 26 yanayounda Uswisi. Majimbo saba tu pekee ndio yalipiga kura ya "hapana".

Karibu pande vyote vya siasa viiliunga mkono pendekezo la serikali. Chama peke cha UDC, ambacho kina idadi kubwa ya wajumbe bungeni kilipinga kizazi cha jamii ya wahamiaji wa Kiislamu, huku kikionyesha mabango yenye lengo la kuchochea uhasama na uchokozi.

Mbunge kutoka chama cha UDC, Jean-Luc Addor, pia mwenyekiti mwenza wa kamati dhidi kurahisishwa kwa uraia, alikubali kushindwa kwake Jumapili kwenye runinga ya RTS.

"Tulikua wachache, na Tatizo la Uislamu, nina hofu kuwa litatukabili katika miaka michache, " amesema mbunge Jean-Luc Addor.

Kamati hii ilikosolewa vikali baada ya kubandika kwenye vituo vya reli na maeneo ya miji yanayotembelewa na watu wengi bango linaloonyesha mwanamke akivaa niqab huku ikiandika: Uraia usiodhibitiwa? Hapana".

"Lengo la kampeni hii ilikuwa kudai utambulisho wa nchi hii na haja ya kuuhifadhi",amesema Jumapili Bw Addor.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.