Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU

Uingereza: kura ya maoni juu ya kuondoka au la katika EU

Zaidi ya Waingeeza milioni 46 wanatarajiwa kupiga kura Alhamisi hii Juni 23 kwa kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Uamuzi ambao unaweza kubadilisha taswira ya historia ya nchi hiyo na ya Umoja wa Ulaya.

Wapiga kura wapanga foleni mbele ya kituo cha kupigia kura London tarehe 23 Juni 2016.
Wapiga kura wapanga foleni mbele ya kituo cha kupigia kura London tarehe 23 Juni 2016. REUTERS/Neil Hall
Matangazo ya kibiashara

Swali ambalo limekua likiulizwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ni kujua , utaratibu utakaotumiwa katika kura hiyo ya maoni.

Baada ya kuingia katika vituo vya kupigia kura leo Alhamisi, wapiga kura watapaswa kujibu swali lifuatalo: "Uingereza inapaswa kubaki mwanachama wa Umoja wa Ulaya au kuondoka katika Umoja wa Ulaya? "Kwa kuchagua" itabidi mpiga kura asahihishe kwenye wneo kunakoandikwa "Remain" ("Kubaki") au "Leave" ("kuondoka").

Wanaruhusiwa kupiga kura wananchi wote wa Uingereza wanaoishi nchini humo. Waingereza wanaoishi nje ya nchi kwa kipindi kisichozidi miaka 15 pia wana haki ya kupiga kura wananchi wa Ireland au raia wa moja ya nchi 53 ya Jumuiya ya Madola anayeishi nchini Uingereza. Utaratibu huu unawapa nafasi raia kutoka mataifa mengine mawili ya Ulaya kupiga kura: Cyprus na Malta.

Vituo vya kupigia kura vitakua wazi kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku saa za Uingereza. Zoezi la kuhesabu kura litaanza baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura na matokeo yanatarajiwa mapema Ijumaa asubuhi.

Muda wa kutangazwa kwa matokeo utategemea na tofauti kati ya kura ya Ndio na Hapana. Kiwango cha ushiriki kinachotarajiwa kutangazwa hivi karibuni, kitatoa muongozo sahihi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.