Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU

Waingereza kupiga kura ya maoni ndani ya siku nne

Waziri Mkuu David wa Uingereza, David Cameron alikuwa usiku wa Jumapili kwenye kituo cha televisheni na redio ya BBC kujibu maswali ya wananchi.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akijibu maswali kutoka kwa wapiga kura wa kambi ya wanaounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa EU na wale kutoka kambi ya wanaotaka nchi hiyo kuondoka katika Umoja huo  kwenye runinga ya Sky News, Juni 2, 2016.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akijibu maswali kutoka kwa wapiga kura wa kambi ya wanaounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa EU na wale kutoka kambi ya wanaotaka nchi hiyo kuondoka katika Umoja huo kwenye runinga ya Sky News, Juni 2, 2016. chris lobina / SKY NEWS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, alirejelea kauli yake kwamba kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya itakua "chaguo litakuepo milele na halitabadilisha, madhara makubwa ya kiuchumi."

David Cameron alitumia nafasi hiyo ya wakati huu wa mwisho kwa raia wa Uingereza kuwakumbusha pointi muhimu ya kampeni yake dhidi ya kutojiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. David Cameron alieleza kuhusu uchumi wa Uingereza bila shaka kuwa utakumbwa na matatizo mengi, lakini pia uhamiaji, suala ambalo limelitikisa bara la Ulaya katika miezi yahivi karibuni.

Alikumbusha kwamba endapo Uingereza itaondoka katika Umoja wa Ulaya, itakuwa vigumu sana kudhibiti wahamiaji na kutakuwa na ukuaji wa kiwango cha chini, ajira chache, na pengu kubwa katika fedha za umma.

"Kama tutakupiga kura kuondoka kwa Uingereza kwa Umoja wa Ulaya, tutakuwa katika hali ya utata kwa karibu muongo mmoja. Miaka miwili ya kujitenga na Umoja wa Ulaya, kisha miaka mingine saba ya kuendesha mazungumzo ya mkataba wa kiuchumi na hiyo ina maana kwamba zaidi ya muongo mmoja bila kujua ni katika mwelekeo gani nchi inaongozwa, " David Cameron alisema.

Alikiri kwamba mjadala ulikuwa mzuri, lakini uligubikwa wakati mwengine na maneno makali, na alikemea hoja za uongo kutoka upande wa kambi inayotaka Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

"Watu wamekua wakipata taarifa za uzushi kwamba Uturuki itajiunga na Umoja wa Ulaya, jambo ambalo ni uongo, kutakuwa na jeshi la Ulaya na kwamba Uingereza itashiriki, jambo ambalo pia ni uzushi, na kuwa utatoa paundi milioni 350 kila wiki kwa Umoja wa Ulaya, uongo vile vile. Sasa kama munataka kupiga kura ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, pigeni kura kwa hiyo, lakini isiwe ni kwa msingi ya hoja hizo tatu ambazo ni za uongo kabisa, " alisisitiza Cameron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.