Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa majimbo: mafanikio ya kihistoria ya chama cha FN

Ikisalia miezi isiopungua 18 ya uchaguzi wa rais, chama cha National Front (FN) kimefanikiwa Jumapili kupata ushindi wa kihistoria katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa majimbo, na kupelekea chama cha PS kujiondoa katika majimbo mawili ambayo kinaona kuwa kitashindwa.

Rais wa chama cha National Front (FN), Marine Le Pen akijibu baada ya kutangazwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa majimbo, Desemba 6, 2015 katika mji wa Henin-Beaumont katika jimbo la Picardie.
Rais wa chama cha National Front (FN), Marine Le Pen akijibu baada ya kutangazwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa majimbo, Desemba 6, 2015 katika mji wa Henin-Beaumont katika jimbo la Picardie. DENIS CHARLET/AFP
Matangazo ya kibiashara

Majimbo hayo ni pamoja na Nord-Pas-de-Calais-Picardie (NPDCP) na PACA.

Chama cha Marine Le Pen kimepata karibu 30% ya kura kitaifa na kudai kuwa ni chama cha kwanza nchini Ufaransa, kinachoongoza dhidi ya chama cha mrengo wa kushoto ambacho kimepata karibu 27% na PS (karibu 23%), kulingana na makadirio ya hivi karibuni.

Orodha ya chama cha FN inaongoza katika majimbo ya Nord-Pas-de-Calais-Picardie, Provence-Alpes-Côte d'Azur, Alsace-Lorraine-Champagne-Ardennes, Midi-Pyrénées, Languedoc-Roussillon, Burgundy-Franche-Comté na katika kanda ya kati.

Katibu wa kwanza wa chama cha PS Jean-Christophe Cambadélis ametangaza kuwa chama chake kimeziondoa orodha zake katika majimbo ya NPDC-Picardie na PACA, akitoa wito wa "kukizuia chama cha Republican", sawa na "kafara" kwa chama cha Kisochalisti, ambacho kwa kipindi cha miaka mitano, hakitashiriki katika shughuli mbalimbali katika majimbo hayo.

Furaha ni tele katika ngome kuu ya Marine Le Pen katika eneo la Henin-Beaumont ikilinganishwa na tamaa na hata kusikitishwa miongoni mwa wapinzani wake wa Republican na hasa PS, ambapo wamekua na huzuni kwa "mkoa huu wa shughuli mbalimbali ambao unastahili bora zaidi."

Mbali na wimbi hili la "bluu" , muungano wa vyama vya Republican-UDI-Modem unaongoza katika mikoa majimbo matatu hadi manne (Pays de la Loire, Auvergne-Rhône-Alpes, Ile de France, Normandy sambamba na chama cha FN). Kwa upande wa chama cha Kisochalisti, kinaongoza katika jimbo la Bretagne, licha ya kampeni ya Jean-Yves Le Drian ambaye jina lake limewekwa nafasi ya kwanza, akihakikisha kuwa atasalia kuwa waziri wa ulinzi, kama vile katika majimbo ya Aquitaine-Limousin- Poitou-Charentes, nyuma ya Alain Rousset.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.