Pata taarifa kuu
TABIA NCHI-UFARANSA-UHAMASISHWAJI

Hali ya hewa: maandamano makubwa kuanzia Sydney hadi London

Maelfu ya watu wameandamana Jumapili hii kutoka nchi mbalimbali dunia, na kutengeneza mlolongo wa watu katika mji wa Paris, ili kupata ahadi dhidi ya ongezeko la joto duniani, siku moja kabla ya mkutano wa kihistoria wa marais na viongozi wa serikali 150.

Maandamano kwa ajili ya hali ya hewa katika mji wa Berlin, Novemba 29, 2015.
Maandamano kwa ajili ya hali ya hewa katika mji wa Berlin, Novemba 29, 2015. JOHN MACDOUGALL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Paris, ambao ulishuhudia mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 130 Novemba 13, maelfu ya watu wameandama, polisi ikishuhudia, kwenye barabara kuu ya Mashariki mwa jiji la Paris licha ya serikali kupiga marufuku kuandamana kufytaia hali ya hatari iliyowekwa.

Kwenye mabango ya waandamanaji kulikua kumeandikwa: "Wanatumia, wanachafua, wanapata faida! Dharura ni ya kijamii na ya kihali ya hewa".

"Natumaini kwamba wakati huu, mkutano huu utachangia kudhibiti hali ya hewa. Sitaki kusikia mwisho wa mkutano huu wanasema tutaandaa mkutano mwingine ", Jean-Pierre Raffin, mwanachuoni mstaafu, na mwanaharakati wa mazingira, amesema.

Justin Trudeau, Waziri mkuu wa Canada, akipokelewa na mwenzake wa Ufaransa Manuel Valls mbele ya ukumbi wa tamasha wa Bataclan, jijini Paris, ambapo mashambulizi ya Novemba 13 yaligharimu maisha ya watu 90.

Maelfu ya viatu yalisambazwa kwenye eneo la Jamhuri, ambapo ungelanzia msafara kwa ajilia ya hali ya hewa, msafara ambao ulifutwa.

Tangu Ijumaa, maandamnao kadhaa yalifanyika duniani kote ili kuweka shinikizo kwa wawakilishi wa nchi 195 watakaokusanya katika eneo la Bourget, kaskazini mwa mji wa Paris, hadi Desemba 11.

Marais na viongozi wa serikali 150 watahudhuria uzinduzi rasmi wa mkutano kuhusu tabia nchi (COP21) utakaofanyika Jumatatu chini ya ulinzi mkali. Mkutano huu wa kilele utatanguliwa Jumapili mchana na mkutano wa kikazi wa wahusika katika katika mazungumzo hayo.

Jumapili hii, watu 45,000 wameandamana katika mji wa Sydney (kusini mashariki mwa Australia), 5000 katika mji wa Adelaide (Kusini) wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamevumilia mvua katika mitaa ya Seoul na mkusanyiko wa watu umeshuhudiwa katika mji wa Delhi.

London, Rio de Janeiro, New York au Mexico kunatazamiwa kuanzishwa upya maandamnao hayo ya kimataifa.

François Hollande atawakaribisha Jumatatu marais na viongozi mbalimbali wa serikali katika eneo la Bourget, ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama, Xi Jinping wa China, Narendra Modi wa India, Vladimir Putin wa Urusi, Recep Erdogan wa Uturuki watafuatana kwenye jukwaa siku nzima kwa dakika chache za hotuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.