Pata taarifa kuu
UFARANSA-KOREA KUSINI-TABIA NCHI

Rais François Hollande ziarani Korea Kusini

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema Jumatano katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, kwamba kugawana teknolojia na nchi kubwa zinazojitokeza kama vile India au China kutaleta "mafanikio au kushindwa" katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi jijini Paris.

Rais Hollande katika mji wa Seoul katika mkutano na vyombo vya habari Novemba 4, 2015.
Rais Hollande katika mji wa Seoul katika mkutano na vyombo vya habari Novemba 4, 2015. AFP/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Changamoto ya Mkutano wa Paris, siyo tu kuweka viwango au vikwazo, lakini pia ni kuchukua changamoto kubwa ya kiteknolojia, ya kutokuwa na hofu ya kuchangia teknolojia. Naamini kile kua hali hiyo itapelekea kushindwa au kufanikiwa ", amesema Rais Hollande katika mkutano na vyombo vya habari, huku akiomba akisisitiza nchi zilizoendelea kuchangia kwa kiwango kikubwa kwa tabia ya nchi duniani.

Kwa mujibu wa Rais Hollande, " kama nchi hazitakua na uhakika kwamba kutakuwa na hatua mpya ya maendeleo kutokana na teknolojia ambayo tunaweza kugawana, nchi hizi hazitowajibika katika zoezi hilo ", Rais Hollande amebaini, akikumbuka kwamba nchi kubwa zinazojitokeza zilisababisha kushindwa kwa Mkutano wa Copenhagen mwaka 2009.

" Inazungumziwa China, India, Brazil, Afrika Kusini, nchi zote ambazo zimeendelea lakini zinataka kuwa na ukuaji endelevu kwa kuzingatia mahitaji yao na ambazo zinatambua wajibu wao wa mazingira lakini zinataka kushindikizwa na zinataka, kufuatia Mkutano kuhusu tabia nchi, kuingia katika masula ya teknolojia ", Hollande amesema akisisitiza.

Hollande ameongea kufuatia mkutano kuhusu tabia nchina ukuaji wa miti na mimea jijini Seoul, wakati wa ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa tangu miaka kumi na tano iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.