Pata taarifa kuu
ULAYA

Umoja wa Ulaya wakubaliana na Uturuki kuhusu wakimbizi

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yanaunga mkono mpango wa Uturuki unaominiwa utasaidia kuwazuia wahamiaji haramu kuingia barani Ulaya.

Meli ya wahamiaji ikiegesha katika kisiwa cha Lesbos, Oktoba 11 2015.
Meli ya wahamiaji ikiegesha katika kisiwa cha Lesbos, Oktoba 11 2015. REUTERS/Fotis Plegas G
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya EU inakuja baada ya zaidi ya watu 600,000 kuhamia barani Ulaya kuanzia mapema mwaka huu.

Serikali ya Uturuki imekubaliana kuanza mazungumzo ya kuwepo kwa VISA kwa wahamiaji watakaotaka kuingia nchini humo.

Hata hivyo, Donald Tusk rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya anasema hatua hiyo ni lazima iangaliwe kwa uangalifu kabla ya kutekelezwa kikamilifu.

Uturuki, imeomba msaada wa Dola Bilioni 3 nukta 4 kuwashughulikia wahamiaji ombalo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema ni wazo zuri.

Kansela Merkel, anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Uturuki kwenda kushauriana na serikali ya Ankara kuhsuu suala hili la wakimbizi.

Rais wa Ufaransa François Hollande naye akizungumzia suala hilo amesema, "hakuna kiwango cha fedha ambacho kimewekwa. Si suala la kutoa fedha. Ni kujua fedha hizo zitatumiwa kwa miradi gani, ".

“ Fedha hizo zitatumiwa kwa kuanzishwa vituo vya wakimbizi na huduma kwa watoto," alisema rais Hollande.

Tume tayari imepanga kutoa "Euro milioni 500 katika fedha zake" ili "kuhakikisha utekelezaji wa mwanzo," amesema Rais wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.