Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi mkuu wafanyika Uingereza

Raia nchini Uingereza wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza leo Alhamisi kuwatafuta viongozi wao.Wabunge 650 watachaguliwa kuingia Bunge la nchi hiyo. Watu milioni 50 wanasadikiwa kuwa walijiandikisha ili kushiriki uchaguzi huo.

Ed Miliband kiongozi wa chama cha Labour, Leanne Wood kiongozi wa chama cha Plaid Cymru, Nicola Sturgeon wa chama cha Scottish National pamoja na et David Cameron kiongozi wa chama cha conservative, katika mjadala uliyorushwa hewani, Aprili 2..
Ed Miliband kiongozi wa chama cha Labour, Leanne Wood kiongozi wa chama cha Plaid Cymru, Nicola Sturgeon wa chama cha Scottish National pamoja na et David Cameron kiongozi wa chama cha conservative, katika mjadala uliyorushwa hewani, Aprili 2.. REUTERS/Ken McKay/ITV
Matangazo ya kibiashara

Takriban vituo vya kupigia kura 50,000 vimefunguliwa nchini kote tangu saa moja asubuhi kwa saa za Uingereza.

Katika uchaguzi huu mkuu, viti zaidi ya 9,000 vya madiwani vinagombewa katika serikali za mitaa 279.

Wakuu wa Kaunti za Bedford, Copeland, Leicester, Mansfield, Middlesbrough na Torbay watachaguliwa pia katika uchaguzi huo.

Saa chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uingereza, viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa wamekua wakizunguka nchi nzima kuhamasisha wapiga kura kwa sera zao za kisiasa.

Vyama vya Conservative na Labour hasa vinataka kujaribu kutafuta kura, ambazo zimekua zikiviweka kwenye nafasi moja tangu miezi kadhaa, karibu asilimia 33 ya kura kila chama.

Viongozi wa vyama na wagombea walifanya kampeni zao za mwisho Jumatano wiki hii kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu Alhamisi wiki hii.

Waziri Mkuu David Cameron aliahidi " kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na " serikali itakayowajali kwanza wafanyakazipamoja na kuokoa mfumo wa Afya, ambao umeendelea kukabiliwa na hali ya sintofahamu".

Kiongozi wa Lib Dem, Nick Clegg aliahidi " hali ya utulivu".

Kura ya maoni inaonyesha kuwa hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.

Kuna uwezekano kuwa uchaguzi huo huenda ukaingia katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja.

Itafahamika kwamba mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.

Vyama mbalimbali tayari vimeanza kujadili ushirikiano ili hali kuna uwezekano mkubwa kwamba hakuna chama kati ya vyama vikuu viwili ambaco kitapata wingi wa kutawala peke yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.