Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Uingereza: mwisho wa kampeni za uchaguzi

Saa chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uingereza, viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa wamekua wakizunguka nchi nzima kuhamasisha wapiga kura kwa sera zao za kisiasa.

Waziri Mkuu David Cameron akiwasili katika mji wa Devon tarehe 5 Mei mwaka 2015.
Waziri Mkuu David Cameron akiwasili katika mji wa Devon tarehe 5 Mei mwaka 2015. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya Conservative na Labour hasa vinataka kujaribu kutafuta kura, ambazo zimekua zikiviweka kwenye nafasi moja tangu miezi kadhaa, karibu asilimia 33 ya kura kila chama.

Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho Jumatano wiki hii kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu Alhamisi wiki hii.

Waziri Mkuu David Cameron ataahidi " kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na " serikali itakayowajali kwanza wafanyakazipamoja na kuokoa mfumo wa Afya, ambao umeendelea kukabiliwa na hali ya sintofahamu".

Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.

Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.

Kuna uwezekano kuwa uchaguzi huo huenda ukaingia katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja.

Itafahamika kwamba mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.

Vyama mbalimbali tayari vimeanza kujadili ushirikianoili hali kuna uwezekano mkubwa kwamba hakuna chama kati ya vyama vikuu viwili ambaco kitapata wingi wa kutawala peke yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.