Pata taarifa kuu
UKRAINE-DEBALTSEVE-USALAMA

Mji wa Debaltseve mikononi mwa waasi

Mji wa Debaltseve na eneo ndogo linalozunguka mji huo vimeanguka mikononi mwa waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine tangu Jumatano Februari 18. Jeshi la Ukraine liliondoka katika mji huo muhimu.

Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine wakiwa kwenye barabara kati ya mji wa Vouglegirsk na Debaltseve, Februari 18 mwaka 2015.
Waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine wakiwa kwenye barabara kati ya mji wa Vouglegirsk na Debaltseve, Februari 18 mwaka 2015. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI, katika mji wa Donbass, Régis Genté, mwaka huu, Ukraine imeendelea kudhoofika kijeshi, licha ya watu wengi kudhihirisha uzalendo wao miezi ya hivi karibuni. Hata hivyo waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki, ambao wamekua wakipewa mafunzo na jeshi la Urusi wanaonekana kuwa na nguvu zaidi na ni wenye adabu.

Kufuatia ushafidi uliyotolewa na wanajeshi wa Ukraine walioondoka katika mji wa Debaltseve Jumatano mchana wiki hii, hakuna kinachofahamika kuhusu kuanguka kwa mji wa Debaltseve mikononi mwa waasi.

Kiev imekua ikilalamikia hali ya mapigano katika mji wa Debaltseve tangu juma lililopita. Viongozi wa Ukraine wamekua wakisema kwamba waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki mwa Ukraine wamekua wakikusanya silaha za kivita na kuziweka pembezoni mwa mji wa Debaltseve. Waasi wamekua wamesha weka nia ya kuudhibiti mji huo.

Waziri wa ulinzi wa eneo lililojitenga la Donetsk, Eduard Basourine, amethibitisha Jumatano jioni kwamba serikali yake imekua ikijiandaa kuondoa silaha za kijeshi katika uwanja wa mapigano, hatua ya pili, baada ya kusitisha machafuko kwa mujibu wa makubaliano yaliyoafikiwa Minsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.