Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UCHAGUZI-CDU-MERKEL-SIASA

Merkel aendelea kupata umaarufu katika CDU

Angela Merkel amechaguliwa tena kwa ushindi wa kishindo kwenye uongozi wa chama chake cha CDU jana, Jumanne Desemba 9, katika mkutano mkuu wa chama hicho uliyofanyika Cologne.

kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amechaguliwa tena kukiongoza chama cha CDU kwa mara ya nane mfululizo, Desemba 9 mwaka 2014.
kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amechaguliwa tena kukiongoza chama cha CDU kwa mara ya nane mfululizo, Desemba 9 mwaka 2014. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo maarufu wa serikali ya Ujerumani kugombea muhula mwengine mwaka 2017.

" Nina furaha kuona hakupata asilimia 101 ya kura. Ingekuwa maajabu, kwa haki", amesema akiwa Brussels waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble, huku akiwa na furaha kufuatia alama alizopata kiongozi wake.

Angela Merkel amepata asilimia 96.7% ya kura dhidi ya asilimia 97.9 alizopata miaka miwili iliyopita. Angela Merkel amejizolea umaarufu tangu alipochukua madaraka ya uongozi wa chama chake cha Christian Democratic Union (CDU) miaka 14 iliyopita.

Kansela Angela Merkel amejizolea umaarufu. Chama chake daima kimekua kikishinda washindani wake kwa zaidi ya asilimia 40% katika uchaguzi. " Angela Merkel ni CDU ; CDU ni Angela Merkel", ndivyo walivyo kuwa wakitamka wafuasi wake baada ya uchaguzi wa jana Desemba 9.

Baada ya ushindi huu, Kansela amejipongeza kufuatia mafanikio ya kiuchumi ya Ujerumani akibaini kwamba chama chake kimekua kikifanya vizuri nchini Ujerumani. Angela Merkel ameanza kuandaa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2017.

Ilikuwa vigumu sana dhidi ya washirika wake katika muungano, jamii ya Wademocrat (SPD). Washirika wake hao walikua wakimpinga ili asiwezi kugomea kwenye uongozi wa muungano wa vyama hivyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.