Pata taarifa kuu

Ujerumani: Berlin yaadhimisha miaka 25 ya kuanguka kwa Ukuta

Nchi ya Ujerumani hii leo Ijumaa Novemba 7 imezindua rasmi wiki ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 25 toka kuangushwa kwa ukuta wa Berlin na kushuhudia kuungana kwa ujerumani Mashariki na Magharibi.

Wakaazi wa mji wa Berlin wakibomoa mabaki ya Ukuta uliyoigawa Ujerumani sehemu mbili, Novemba 16 mwaka 1989.
Wakaazi wa mji wa Berlin wakibomoa mabaki ya Ukuta uliyoigawa Ujerumani sehemu mbili, Novemba 16 mwaka 1989. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye yeye mwenyewe anatokea upande wa mashariki ya Ujerumani anatarajiwa kuongoza sherehe hizi za siku tatu kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wakijaribu kuruka ukuta kutoka kwenye eneo hilo November 9 mwaka 1989.

Maadhimisho haya yaliyopewa jina “Uhuru thabiti” yanakumbukwa kama mapinduzi ya amani yaliyoshuhudia utawala wa kikomunist wa Ujerumani mashariki ukifungua rasmi mipaka ya nchi hiyo baada ya kuwa imefungwa kwa zaidi ya miaka 28 ambapo wananchi wake walikuwa wafungwa ndani ya nchi yao.

Maandamano makuu yamepangwa kufanyika mbele ya lango la Brandenburg Jumapili kuanzia saa 14 mchana saa za Ujerumani. Wasanaii wengi wa Ujerumani ikiwa ni pamoja na wale kutoka eneo la Magharibi na Mashariki na wasanii kutoka mataifa ya kigeni watashiriki maandamano hayo.

Viongozi wawili wa Ujerumani Mashariki ya Ujerumani ya mwaka 2014, Rais Joachim Gauck na Kansela Angela Merkel watashirikia pia maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.