Pata taarifa kuu
VATICAN-KOREA KUSINI-Dini

Vatican : Papa Francis ziarani Asia

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa francis amewasili hii leo jijini Seoul nchini Korea Kusini, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa kanisa katoliki barani asia kwa kipindi cha miaka 15 yenye lengo la kuboresha uhusiano ya madhehebu ya katoliki barani humo lakini pia kutetea maridhiano baina ya watu wa Corea.

Papa Francis akiwasili katika mji mkuu wa Corea Kusini, Seoul, alhamisi Agosti 14 2014.
Papa Francis akiwasili katika mji mkuu wa Corea Kusini, Seoul, alhamisi Agosti 14 2014. REUTERS/Hwang Gwang-mo/Yonhap
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya mwisho ya kiongozi wa kanisa katoliki barani Asia ilikuwa ni ya Papa John Paulo wa pili ambaye alitembelea nchini India mwaka 1999, na sasa ni miaka 15 kiongozi wa kanisa katoliki anatembelea bara hilo lenye waumini takribani asilimia 3.2 wa kanisa katoliki.

Watalam wanaona kuwa ziara ya Papa ni ishara ya nguvu ya utambuzi wa uongozi wa Vatican kuwa Kanisa katoliki limeendelea kukuwa kwa kasi katika bara la Asia na eneo la kusini mwa jangwa la sahara.

Kutokana na tofauti ya muda, agenda ya ziara hiyo katika siku ya kwanza imealazimika kurekebishwa ambapo Papa atakutana katika sherehe zitazo hudhuriwa na rais mbele ya viongozi 800 wa nchi kabla ya kukutana na maaskofu 35.

Malengo ya ziara hiyo yaliwekwa wazi na uongozi wa Vatican ambapo kwanza kabisa ni kutowa ujumbe wa Uinjilisti katika bara la Asia lenye kuwakilisha asilimia 3.2 ya wakatoliki, kutoa ujumbe kwa vijana waumini wa kanisa katoliki wanaokutana katika siku ya vijana wa kikatoliki kutoka mataifa 23 barani humo, lakini pia waumini wa Kanisa katolika wa china pia watatembelewa na baba Francis.

Kiongozi nambari mbili wa Vatican Pietro Parolin amesema Papa Franics ametowa ujumbe kwa mataifa yote barani Asia ambapo amezungumzia kuhusu hatma ya Asia.

Papa Francis atatowa hotuba 11 kwa lugha za kitaliana na kingereza ambapo anasubiriwa kuhubiria kesho katika sherehe za kukumbuka kupaa mbinguni kwa bikira Maria, sanjari na siku kuu ya kitaifa nchini Korea Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.