Pata taarifa kuu
Israeli-Palestina

Papa Francis adiriki ibada ya pamoja na ma rais Shimon Peres na Mahmoud Abbas

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kanisa katoliki, kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis amefanya sala ya pamoja na rais wa Israel Shimon Peres na rais wa mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas, kwenye tukio lililolenga kuwaleta pamoja vongozi hao.

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis na ma rais Shimon peres wa Israeli pamoja na Mahmoud Abbas wa Palestina
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis na ma rais Shimon peres wa Israeli pamoja na Mahmoud Abbas wa Palestina
Matangazo ya kibiashara

Ma rais Shimon Peres (G) na Mahmoud Abbas wakipeana mkono huku Papa Francis akiangaliauin 2014.
Ma rais Shimon Peres (G) na Mahmoud Abbas wakipeana mkono huku Papa Francis akiangaliauin 2014. REUTERS/Max Rossi

Akizungumza mara baada ya kufanya sala ya pamoja na viongozi hao, papa Francis hakusita kutoa wito kwa pande hizo mbili kumuogopa Mungu na kuhakikisha wanapata suluhu ya kudumu kwenye eneo lao na eneo zima la mashariki ya kati.

Papa Francis amesema maombi haya wala mkutano wake na viongozi wa Israel na Pa

lestina hayakuwa kisiasa lakini ni kujaribu kuwajengea imani kuhusu umuhimu wa amani.

Kwenye hotuba yake rais wa Israel Shimon Peres amekiri kukerwa na mzozo unaoendelea kati yake na Palestina na kwamba anatamani siku moja kuona mzozo huu ukiisha.

Kwa upande wake rais wa mamlaka ya palestina, Mahamoud Abbas amesema kuwa nchi yake inataka kuona amani kati yake na Israel inapatikana ili kuwaondolea shida wananchi wa Palestina.

Kwenye maombi haya, papa Francis alijumuika pamoja na viongozi wa madhehebu ya Coptic, Othoerdox na wale wa kiislamu ambao walifanya sala pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.