Pata taarifa kuu
UHOLANZI-UKRAINE-Usalama wa anga

Ukraine : miili mingine ya wahanga yatazamiwa kusafirishwa Uholanzi

Baada ya miili zaidi ya 40 ya wahanga waliofarika katika ajali ya ndege ya Malaysia Ainlines kusafirishwa hapo jumatano wiki hii nchini Uholanzi, miili mingine inatazamiwa kusafirishwa alhamisi hii kutoka katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine.

Baadi ya mabaki ya MH17 ya  Malaysia Airlines, karibu na kijiji cha Grabovo,katika eneo la Donetsk, Julai 21 mwaka 2014.
Baadi ya mabaki ya MH17 ya Malaysia Airlines, karibu na kijiji cha Grabovo,katika eneo la Donetsk, Julai 21 mwaka 2014. REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

Hata hivo Umoja wa Ulaya unapanaga kuzidisha vikwazo dhidi ya Urusi amabayo inatuhumiwa kusaidia na kuwafadhili waasi mashariki mwa Ukraine.

Mabalozi wa mataifa 28 wanakutana tangu asubuhi mjini Brussels ili kujadili majina mapya ya viongozi wa Urusi ambao wanalengwa kuchuliwa vikwazo kutokana na kuwaunga mkono waasi mashariki mwa Ukraine.

Hapo jumatano wiki hii, wiki moja baada ya ajali ya boeing 777 ya Malaysia Airlines kufuatia shambulio la kombora, ndege mbili za jeshi la Ukraine zimedunguliwa eneo lilioko kilomita zaidi ya 10 na eneo la kulikodunguliwa ndege hiyo ya Malaysia Airlines. Kiev imebaini kwamba ndege hizo zimedunguliwa na makombora yaliyofyatuliwa kutoka upande wa Urusi.

Awali Marekani ilifahamisha kwamba ndege ya Malaysia Airlines ilidunguliwa bila kukusudiwa na waasi mashariki mwa Ukraine wakiwa katika mafuzo ya kijeshi.
Lakini Urusi iliituhumu hivi karibuni Ukraine kuhusika katika udunguwaji wa ndege hiyo MH17. Muhusika hajajulikana hadi leo lakini uchunguzi unaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.