Pata taarifa kuu
URUSI-AUSTRIA-IRAN-Diplomasia

Urusi : Sergueï Lavrov hatoshiriki mkutano mjini Vienna

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchini zenye nguvu duniani watakutana jumpili wiki hii katika mji mkuu wa Austria, Vienna kuzungumzia mpango wa nuklia wa Iran, amethibitisha mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, ambaye ndiye anayesimamia mazungumzo hayo.

Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi.
Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Catherine Ashton amewaalika mawaziri watakaokua na muda kushiriki mkutano huo ili kutathmini kwa pamoja wapi mazungumzo kuhusu mpango huo wa Iran umefikia, msemaji wa Catherine Ashton, Michael Mann amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mazungumzo kati ya Iran na mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la mataifa sita, ambayo ni Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Urusi na China, yaliyoanza tangu juma liliyopita, yana lengo la kupatikana kwa mkataba unaotoa matumaini kwamba mpango huo wa Iran ni salama kwa mataifa mengine.

Iwapo watafikiya mkataba huo, Iran itaondolewa vikwazo viliyochukuliwa na jumuiya ya kimataifa, ambavyo vinaathiri uchumi wa taifa hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imethibitisha kwamba John Kerry atajielekeza mwishoni mwa juma mjini Vienna ili kujaribu kuonesha mtafaruku uliopo ambao unapaswa kujadiliwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry .
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry . REUTERS/Jacquelyn Martin

Hata hivo, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergueï Lavrov, amesema hatoshiriki mkutano huo.

“Waziri hatoshiriki mkutano, na wameniomba nihudhuriye mkutano huo”, mwakilishi wa kudumu wa Urusi kwenye taasisi za kimataifa mjini Vienna, Vladimir Voronkov, ameambia kituo cha habari cha serikali Itar-Tass.

Voronkov, amejieleza kuwa Sergueï Lavrov atakua ameambatana na rais Vladimir Poutine katika ziara ya kikazi katika mataifa ya Amerika ya kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.