Makubaliano kati ya Marekani na Taliban ya kubadilishana wafungwa, yahojiwa
Hatau ya kundi la Taliban, Qatar na nchi ya Marekani kufukia makubaliano kwa kubadilishana wafungwa hao wa Taliba kwa mwanajeshi mmoja wa Marekani aliyikuwa anashikiliwa kwa zaidi ya miaka mitano na kundi hilo, imeibua maswali kuhusu sera ya Qatar na kundi la Taliban.Β
Imechapishwa:
Serikali ya Marekani imesema kuwa tayari wamempokea mwanajeshi wao, Sajenti Bowe Bergdahl ambaye alisafirishwa hadi nchini Ujerumani kwenye hospitali ya jeshi la Marekani kwa uchunguzi zaidi wa kiafya.
Uamuzi huu wa kubadilishana wafungwa wa Taliban na mwanajeshi wa Marekani, ilisimamiwa na nchi ya Qatar ambayo imesema makubaliano haya yalitokana na sera yake ya kuheshimu haki za binadamu bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Akizungumza saa chache baada ya mwanajeshi huyo kuachiliwa, rais Barack Obama akiwa na wazazi wa mwanajeshi huyo kwenye ikulu ya Washington, amesema kuwa Bowe alikosa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na mapumziko na kwamba Serikali yake haikufanya vyakutosha kuhakikisha anaachiliwa huru.
Rais Obama ametoa pongezi kwa mfalme wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani pamoja na utawala wa Kabul kwa kuhusika moja kwa moja katika kuhakikisha mwanajeshi hiyo anaachiwa huru.
Serikali ya Qatar hapo jana wakati ikijibu maswali ya waandishi wa habari, ilikataa katukatu kuweka wazi misingi ya kuachiwa kwa viongozi hao wa Taliban ambao walikamatwa wakati wa vita ya kulisambaratisha kundi hilo nchini Afghanistan.
Hatua hii imeibusha maswali mengi toka kwa wanaharakati ambao wanadai kuwa huenda viongozi hao wakarejea uraiani na kuanza tena harakati zao za kuipinga Serikali ya Afghanistan.
Utawala wa Qatar umesema kuwa licha ya viongozi hao kuachiwa huru, kuna hatua ambazo wao watazichukua kama nchi kuhakikisha hawarejei kwenye harakati zao na kundi la Taliban.