Pata taarifa kuu
MAREKANI-PAKISTAN

Marekani yakanusha kukwamisha mazungumzo ya amani baina ya Pakistan na Taliban

Marekani imetupilia mbali madai ya kuwa imekuwa kikwazo dhidi ya jitihada za mazungumzo ya amani baina ya serikali ya Pakistan na wanamgambo wa Taliban. Washington imekanusha madai hayo ambayo yamechochewa na kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Tehreek-e-Taliban nchini Pakistan Hakimullah Mehsud aliyeuawa katika shambulio la ndege zisizokuwa na rubani mjini Waziristan siku ya ijumaa.

REUTERS/Reuters TV/Files
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Washington imeendelea kusisitiza kuwa wao wana lengo moja na Pakistan ambalo ni kukomesha ugaidi.

Awali Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Chaundry Nisar alilaumu mashambulizi hayo yanayofanywa na vikosi vya Marekani na alilitaja shambulizi lililosababisha kifo cha kiongozi huyo kama kizingiti kilichokuja siku chache kabla ya pande hizo mbili kuanza mazungumzo.

Majeshi ya usalama nchini Pakistan yapo katika tahadhari ya hali ya juu yakihofia huenda Taliban ikalipiza kisasi baada ya kuuawa kwa kiongozi wao.

Katika hatua nyingine Marekani imethibitisha kuwa Balozi wake Richard Olson amehojiwa na Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan, ingawa haijaweka wazi kilichojadiliwa katika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.