Pata taarifa kuu
Uingereza

Kocha wa Liverpool hafikirii kujiuzulu licha ya timu yake kususua

Kocha wa Klabu ya Uingereza ya Liverpool Kenny Dalglish hatajiuzulu pamoja na timu yake kususua katika ligi kuu ya Uingereza na kombe la FA.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo ni kwa mjibu wa mtu wake wa karibu na mchezaji mwenzake wa zamani Mark Lawrenson ambaye amesema kocha huyo hafikirii kufanya uamuzi wa kung'oka katika klabu hiyo.

Amesema kuwa haamini hata kama klabu hiyo itamfurusha kocha huyo kutokana na Liverpool kufanya vibaya kwa kupata vipigo vya mfululizo.

Itakumbukwa kuwa Liverpool ilishinda kombe la Carling na sasa ipo katika hatua za nusu fainali za Kombe la FA lakini vipigo mfululizo ndivyo vinatia wasiwasi kama timu hiyo itafanya vizuri ama la.

Kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa New Castle katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kilikua ni sita mfululizo katika mechi za ligi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.