Pata taarifa kuu
Ufaransa-Uchaguzi

Nicolas Sarkozy asema kuna wahamiaji wengi nchini Ufaransa

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akiwa katika kampeni za uchaguzi,  amesema kwamba nchini Ufaransa kuna wahamiaji wengi mno, na ameahidi kupunguza idadi ya wakimbizi wapya kufikia nusu ya waliopopo sasa.

Nicolas Sarkozy Rais wa Ufaransa
Nicolas Sarkozy Rais wa Ufaransa Reuters / Eric Feferberg
Matangazo ya kibiashara

Nicolas Sarkozy amesema mfumo wa muingiliano nchini Ufaransa unafanya kazi vibaya kwa sababu kuna wageni wengi sana, hali ambayo inapelekea wengi kukosa malazi, kazi na shule.

Sarkozy amekuwa akituhumiwa na upinzani kutumia fursa hiyo ya kampeni na kuleta maswala ambayo yanazua utata nchini Ufaransa akitaka kujizolea kura nyingi kwa katika duru ya kwanza ambayo imepenagwa kufanyika April 22.

Kwa kipindi cha miaka mitano Sarkozy amesema ataanzisha upya mchakato wa ushirikiano katika mazingira mazuri, na lazima kugawanya mara mbili idadi ya watu kutoka 180,000 kwa mwaka hadi 100,000," alisema.

Sarkozy pia alitangaza mipango mipya ya kupunguza baadhi ya malipo ya faida ya ustawi wa sasa inapatikana kwa wafanyakazi wahamiaji kwa wale ambao walifurahia ukaazi kwa miaka 10 na kuwa na kazi kwa ajili ya wale wa miaka tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.