Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-UAE-URUSI-UCHUMI

Saudi Arabia na UAE waongeza shinikizo, bei ya mafuta yapungua

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, washirika wawili wakuu katika Shirika la Nchi zinazosafirisha kwa wingi mafuta duniani, OPEC, wameongeza shinikizo katika vita vya bei ya mafuta wanayoagiza Urusi, na kutangaza kwamba wanaweza kufurika masoko ya duniani kwa bidhaa hiyo, ambayo bei yake imeshuka leo Jumatano.

Abiria katika ndege anaangalia kiwanda cha Joubeil, Mashariki mwa Saudi Arabia Desemba 11, 2019.
Abiria katika ndege anaangalia kiwanda cha Joubeil, Mashariki mwa Saudi Arabia Desemba 11, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia, ambayo ni kiongozi wa Shirika la Nchi Zinazosafirisha Petroli (OPEC), imeendelea kufanya ushawishi ili Urusi - ambayo ni mzalishaji wa pili mkubwa duniani lakini sio mwanachama wa OPEC - kukubali kupunguza uzalishaji wa mafuta ghafi duniani ili kulipa fidia ya punguzo kwa mahitaji yanayosababishwa na mripuko wa ugonjwa mpya wa Covid-19.

Awali taarifa za vyombo vya habari zilisema Shirika la Nchi Zinazosafirisha kwa Wingi Mafuta Duniani-OPEC, limeshindwa kufikia makubaliano na Urusi na nchi zingine zisizo wanachama wa OPEC juu ya mpango wake wa kupunguza uzalishaji zaidi wa mafuta ghafi.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa Urusi ilipinga kuunga mkono mpango huo na maafisa walishindwa kukubaliana juu ya kuongeza muda kupunguza uzalishaji ambao umeendelea kwa miaka mitano iliyopita kusaidia kuwepo kwa bei nzuri.

Bei za mafuta ghafi duniani zilishuka kutokana na mlipuko wa virusi vya korona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.