Pata taarifa kuu
AFRIKA-MAURITIUS-UCHUMI

Ripoti: Watu binafsi na mashirika mbalimbali yanatumia mauritius kwa kukwepa kulipa kodi

Uchunguzi mpya uliofanywa hivi karibuni unaonesha namna mataifa masikini barani Afrika yanavyoendelea kupoteza mamilioni ya fedha za mapato ya kodi kutoka kwa makampuni ya kimataifa na watu matajari.

Makao makuu ya Bunge, Port-Louis, Mauritius, nchi ambayo inastumiwa kutumiwa na makampuni mbalimbali na watu binafsi kwa kukwepa kulipa kodi..
Makao makuu ya Bunge, Port-Louis, Mauritius, nchi ambayo inastumiwa kutumiwa na makampuni mbalimbali na watu binafsi kwa kukwepa kulipa kodi.. Karsten Ratzke/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na shirika la kimataifa la waandishi wa habari wa uchunguzi, makampuni na watu binafsi wamekuwa wakitumia visiwa vya Mauritius kukwepa kulipa kodi kubwa katika nchi ambako wanatengeneza fedha zao.

Serikali ya Mauritius hata hivyo imekanusha tuhuma za kukiuka sheria za kimataifa ikisisitiza kushirikiana na kuheshimu sheria za kimataifa kuhusu kodi.

Ripoti hii ya nyaraka zaidi ya laki 2 za siri, imeonesha namna kampuni moja ya wanasheria ikiyasaidia makampuni na watu binafsi kukwepa kulipa mamilioni ya kodi.

Nyaraka hizo za siri kutoka katika barua pepe, vinoti na barua, iliyopewa jina la Mauritius Leaks, imeonesha namna makampuni hayao yanakwepa kodi kutoka katika nchi masikini barani Afrika, Mashariki ya kati na Asia Kusini kwaajili ya kuyanufaisha makampuni ya nchi za magharibi huku Mauritius ikinufaika na mgao.

Uchunguzi huu umefanyika kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2017 na unakuja baada ya kashfa nyingine ya Panama Papers mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.