Pata taarifa kuu
UFARANSA-NIGERIA-USALAMA-SIASA-UTAMADUNI

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron azuru Nigeria

Baada ya Mauritania, ambako alihudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika na kujadili masuala ya usalama kuhusu kikosi cha kikanda katika eneo la Sahel, G5 Sahel, Emmanuel Macron amekua akitarajiwa Jumanne hii, Julai 3 nchini Nigeria.

Emmanuel Macron na Muhammadu Buhari mnamo Desemba 12, 2017 Paris, Ufaransa.
Emmanuel Macron na Muhammadu Buhari mnamo Desemba 12, 2017 Paris, Ufaransa. ALAIN JOCARD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya rais wa Ufaransa nchini Nigeria inaangaziwa katika masuala matatu: siasa, uchumi na utamaduni.

Kwa upande wa rais wa Ufaransa, Nigeria kwanza ni chaguo la kihisia. Macron aliwahi kuishi nchini Nigeria kwa miaka 15 akifanya kazi katika Ubalozi wa Ufaransa.

Nigeria pia ni chaguo la kisiasa kutokana na hadhi ya rais Muhammadu Buhari katika eneo la Afrika Magharibi. Hakuna shaka kwamba viongozi hawa wawili, Jumanee hii Julai 3, hawatazungumzia tukuhusu mapambano dhidi ya Boko Haram lakini pia kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Togo.

Rais Emmanuel Macron anatarajiwa pia kutembelea mjini Lagos na kwenda katika kilabu ya usiku iliyoanzishwa na aliyekuwa mwanamuziki maarufu Fela Kuti.

Fela Kuti alifariki dunia mwaka 1997 lakini mtoto wake Femi atampokea rais wa Ufaransa pamoja na wanamuziki wengine nguli kutoka Afrika, kama vile Youssou N'Dour na Angélique Kidjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.