Pata taarifa kuu
ALGERIA-RUSHWA-SIASA

Mkuu wa polisi atimuliwa kwenye wadhifa wake Algeria

Mkuu wa Polisi nchini Algeria Abdelghani Hamel amefutwa kazi na ofisi ya rais nchini humo. Hatua hii imewashangaza wengi nchini Algeria. Kufutwa kwake kunaelezewa kuwa ni katika muktadha wa mapambano kuhusu mtu atakayemrithi rais wa nchi hiyo Abdelaziza Bouteflika.

Abdelghani Hamel alikuwa mtu wa karibu wa Abdelaziz Bouteflika (kwenye picha).
Abdelghani Hamel alikuwa mtu wa karibu wa Abdelaziz Bouteflika (kwenye picha). © Canal / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii mshirika huyu wa karibu wa Abdelaziz Bouteflika alishtumu kuepo na kashfa ya rushwa katika uchunguzi wa biashara ya madawa ya kulevya aina ya cocaine, huku akiwashtumu maafisa kadhaa wa idara za usalama.

Abdelghani Hamel alikuwa mtu wa karibu na Abdelaziz Bouteflika, lakini amechukuliwa hatua ya kufutwa kazi. Awali alishtumu polisi kushindwa kukabiliana na biashara haramu ya madawa ya kulevya katika bandari ya Oran. Lakini pia alisema: "Yeyote anayehusika na vita dhidi ya rushwa lazima awe msafi".

Hata hivyo, siku tatu kabla, Waziri wa Sheria alitangaza kuwa wizara yake itachunguza kuhusu kesi za rushwa zinazohusiana na biashara ya madawa ya kulevya aina ya cocaine.

Haya ni mashambulizi dhidi ya maafisa wengine katika nchi hiyo ambayo yamesababishwa mkuu wa polisi anafutwa kazi. Wakati huo huo chanzo kilio karibu na ofisi ya rais kinasema kuwa afya ya rais Bouteflika imeendelea kudorora na kwamba mwisho wa muhula wake umefika, maandalizi ya kumpata mrithi wake yanaendelea kuzua sintofahamu nchini Algeria.

Waziri Mkuu wa zamani, Abdelmadjid Tebboune, alipoteza wadhifa wake wakati wa majira ya joto baada ya kutangaza kuanzisha uchunguzi kwa wafanyabiashara walio karibu na utawala.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.