Pata taarifa kuu
ISRAEL-UFISADi-UCHUMI

Waziri Mkuu wa Israel ahojiwa na polisi

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesilikizwa leo Ijumaa kwa mara ya kwanza na polisi kuhusu uchunguzi unaohusiana na madai ya rushwa yanayohusisha Bezeq, kampuni kuu ya mawasiliano ya simu nchini Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aendelea kukabiliwa na shutma za rushwa.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aendelea kukabiliwa na shutma za rushwa. REUTERS/Gali Tibbon
Matangazo ya kibiashara

Polisi wa Israeli waliwasili katika makazi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu leo Ijumaa ili kumsikiliza kuhusu kesi ya rushwa inayomkabilia kwa mujibu vyombo vya habari nchini humo

Polisi wanawashtumu wamiliki wa kampuni ya Bezeq Telecom kuchapisha makala kwa faida ya Benjamin Netanyahu na mkewe kwenye tovuti ya habari wanayodhibiti baada ya kukubaliwa mambo fulani na mamlaka inayodhibi mawasiliano nchini humo.

Benjamin Netanyahu, ambaye pia anakabiliwa na kesi nyingine mbili za rushwa, aamekanusha kuhusika na ufisadi wowote.

Kesi mbili za rushwa zinazomkabili zinatishia utawala wake wa muda mrefu.

Mwandishi wa habari wa AFP aliona magari mawili ya polisi yakiingia katika makazi yake mjini Jerusalem karibu saa tatu asubuhi (saa za Israel).

Mkewe, Sara Netanyahu, atahojiwa katika kituo cha polisi, kulingana na taarifa za vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.