Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Rais Zuma aendelea kushinikizwa kujiuzulu

Maafisa wa juu wa chama cha ANC walikutana kwa mazungumzo na Rais wa Afrika Kuini Jacob Zuma na kumtaka ajiuzulu kwenye wadhifa wake kufuatia madai ya rushwa yanayomkabiuli na hivyo kusababisha wafuasi wengi kukihama chama hiki tawala nchini humo.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kufuatia kashfa za rushwa zinazomkabili.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kufuatia kashfa za rushwa zinazomkabili. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulifanyika Jan Jumapili, na hivi leo maafisa vigogo na wae wenye ushawishi mkubwa katika chama wanatarajia kufanya mkutano wa dharura.

Mpaka sasa haijafahamika hatua ambayo itachukuliwa. Lakini katika mkutano wa jana Jumapili maafisa karibu wote walishiriki mkutano huo walionekana kuwa wamechoshwa na madai ya ufisadi yanayomkabili Zuma.

Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.

Duru kutoka chama cha ANC zinasema kuwa vigogo wa chama wana wasi wasi kuwa hali hiyo inaweza kukigawa chama kama hakuna hatua itakayochukuliwa haraka iwezekanavyo kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Maafisa wakuu katika chama cha ANC wanatarajiwa kuanza utaratibu wa kumuondoa madarakani kwa kuidhinisha hoja bungeni au kupia mfumo rasmi.

Chama cha ANC kimepoteza umaarufu wake katika muhula wa pili wa Jacob Zuma, wakati ambapo mdororo wa uchumi unaendelea kushuhudiwa, huku Rais Zuma akiendelea kukabiliwa na tuhuma za rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.