Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIASA-UCHUMI

Rais mteule wa Liberia aahidi kubadilisha sheria za uraia

Rais mteule wa Liberia George Weah ameagiza kutolewa kwa kipengele kinachoonyesha ubaguzi kwenye katiba ya nchi hiyo, ambacho kinaruhusu upatakanaji wa uraia kwa watu weusi tu.

Rais wa Liberia, George Weah, Disemba 30, 2017.
Rais wa Liberia, George Weah, Disemba 30, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kwanza ya taifa tangu achaguliwe kuwa Rais wa Liberia.

Weah amesema vikwazo na vipingamizi vyote hivi viliwekwa wakati ambao havikuwa vinahitajika tena.

“Kipengele hicho ni cha baguzi na hakina maana yoyote'' Rais Weah amesemahotuba yake ya kwanza ya taifa tangu achaguliwe kuwa Rais.

Katiba inamtambulisha mtu mweusi ''Negro'' jina la kibaguzi walilokuwa wakiitwa watu weusi wakati wa utumwa.

George Weah ameahidi pia kufuta sheria inayowazuia wenyeji kumiliki ardhi.

Watu kutoka mataifa mbalimbali hasa raia 4,000 wa Lebanon wanaishi nchini Liberia kwa miongo kadhaa, lakini amenyimwa uraia na haki ya kumiliki ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.