Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHAGUZI-SIASA

Rais Mugabe amfuta kazi makamu wake

Siku moja baada ya mkewe Rais Robert Mugabe, Grace Mugabe kutaka sheria za chama zirejelewe upya ili aweze kuchukua nafasi ya makamu wa rais, kwa lengo la kumrithi mumewe, hatimaye Rais Mugabe amemfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa.

Emmerson Mnangagwa aliteuliwa kuwa makamu wa rais mwaka 2014, akichukua nafasi ya Joice Mujuru, aliyepoteza nafasi yake baada ya kampeni ya Grace Mugabe ambaye alimshtumu kuwa anataka kumpindua rais Mugabe.
Emmerson Mnangagwa aliteuliwa kuwa makamu wa rais mwaka 2014, akichukua nafasi ya Joice Mujuru, aliyepoteza nafasi yake baada ya kampeni ya Grace Mugabe ambaye alimshtumu kuwa anataka kumpindua rais Mugabe. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kufutwa kwake ni ishara kuwa Grace Mugabe, atafuata nyayo za mumewe za kuwa rais wa Zimbabwe.

Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 75, ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Bw. Mnangagwa ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais, kwamujjibu wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo.

Siku ya Jumapili, Grace Mugabe pia alimshtumu Emmerson Mnangagwa kupanga njama, ikiwa ni pamoja na mapinduzi ya kijeshi wakati wa sherehe za uhuru. "Mwaka 1980, mtu huyu aitwaye Mnangagwa alitaka kufanya mapinduzi ya kijeshi. Alitaka kuchukua mamlaka ya rais. Alikuwa na uhusiano na wazungu", Grace Mugabe alisema.

Rais Robert Mugabe alisikika siku moja kabla kuwa anaweza kumfukuza kazi Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye anaonekana kama mmoja wa warithi wake na ambaye pia anaonekana kuwa mpinzani wa mke wa Rais Mugabe.

Emmerson Mnangagwa, anayejulikana kwa jina maarufu la "mamba", tayari alipoteza nafasi yake ya Waziri wa Sheria mapema mwezi Oktoba. Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, alisema chama tawala hivi karibuni kitabadili sheria zake ili mwanamke awe makamu wa rais.

Emmerson Mnangagwa aliteuliwa kuwa makamu wa rais mwaka 2014, akichukua nafasi ya Joice Mujuru, aliyepoteza nafasi yake baada ya kampeni ya Grace Mugabe ambaye alimshtumu kuwa anataka kumpindua rais Mugabe.

Chama tawala, Zanu-PF, kinakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kuhusu mrithi wa Robert Mugabe, ambaye alikataa kuteua mrithi. Rais Mugabe tayari ametangaza kwamba atawania muhula mwingine katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.