Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA

FIFA: Viwanja 4 tayari kwa kuandaa fainali ya Kombe la Dunia 2018

Shirikisho la soka duniani FIFA, linasema viwanja vinne vipo tayari kuandaa fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Uwanja wa Luzhniki ambao umekuwa ukikarabatiwa, utafunguliwa rasmi tarehe 11 mwezi Novemba, wakati wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki kati ya wenyeji Urusi na Argentina.
Uwanja wa Luzhniki ambao umekuwa ukikarabatiwa, utafunguliwa rasmi tarehe 11 mwezi Novemba, wakati wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki kati ya wenyeji Urusi na Argentina. REUTERS/Arnd Wiegmann/Files
Matangazo ya kibiashara

Viwanja hivyo ni pamoja na Spartak Stadium, Kazan Arena, Saint Petersburg Stadium na Fisht Stadium vyote vilivyoandaa michuano ya Shirikisho mwaka huu.

Uongozi wa soka nchini Urusi unasema ukarabati katika viwanja huu umekamilika na hata michuano ya ligi kuu inaendelea kushuhudiwa.

Uwanja wa Luzhniki ambao umekuwa ukikarabatiwa, utafunguliwa rasmi tarehe 11 mwezi Novemba, wakati wa mchuano wa Kimataifa wa kirafiki kati ya wenyeji Urusi na Argentina.

Mwaka 2013, ukarabati wa uwanja huo ulianza, ikiwa ni pamoja na kupanda nyasi mpya na kuongeza idadi ya viti na kupendezesha eneo la kuketi mashabiki.

Huu ni uwanja ambao umewahi kuandaa michezo ya Olimpiki mwaka 1980.

Luzhniki ndio ukaoakuwa uwanja mkuu wa mashindano haya mkubwa kutokana na uwezo wa kuruhusu mashabiki 81,000.

Timu ya taifa ya nyumbani, ambayo ni Urusi itafungua mchuano wake wa kwanza katika kundi A, katika uwanja huo uliopo jijini Moscow ambao utaanda fainali ya michuano hiyo.

Krestovsky ni uwanja mwingine mkubwa unaoapatikana mjini Saint Petersburg ambao una uwezo wa kuwaruhusu mashabiki 68,134.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.