Pata taarifa kuu
DRC, SIASA

Serikali mpya DRC yatawazwa, wabunge wa rassemblement wasusia

Bunge la taifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeidhinisha na kutawaza serikali mpya inayoongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala. Baada ya kikao hicho, wabunge waliidhinisha mpango wa serikali.

Waziri Mkuu mpya wa DRC, Bruno Tshibala, Aprili 4, 2017, Kinshasa.
Waziri Mkuu mpya wa DRC, Bruno Tshibala, Aprili 4, 2017, Kinshasa. JUNIOR KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla ya wabunge 337 ambao walishiriki katika kikao cha bunge siku ya Jumane Mei 16, 336 waliidhinisha mpango wa serikali, mmoja pekee hakupiga kura.

Aubin Minaku, Spika wa Bunge, alimuomba Waziri Mkuu kuwasilisha haraka, muswada wa sheria kuhusu bajeti ya mwaka 2017 ya serikali mpya.

Katika kuwasilisha mpango wa serikali yake, Waziri Mkuu mpya Bruno Tshibala alizungumzia mambo manne ambayo serikali yake itaharakia kufanya.

Maandalizi ya uchaguzi ndani ya kipindi walichokubaliana, kurejesha hali ya utulivu na kuinua uchumi wa taifa, kuboresha hali ya maisha ya wananchi na kuimarisha usalama wa watu na mali zao.

Alisisitiza hasa kuhusu maandalizi ya uchaguzi, akiwaahidi wananchi wa DRC kwamba atahakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira mazuri na itakua ni uchaguzi mzuri katika historia ya nchi hiyo.

Hata hivyo katika kikao hicho cha Bunge, wabunge kutoka muungano wa upinzani wa Rassemblement wanaomuunga mkono wamesusia kikao hicho cha kutawazwa kwa serikali mpya inayoongozwa na Bruno Tshibala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.