Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON-SIASA

Macron kumteua waziri wake mkuu Jumatatu

Wakati ambapo Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa Jumatatu hii Mei 15 kumteua waziri wake mkuu, tayari washirika wake wa karibu wametoa majina ya sehemu ya kwanza ya maafisa wa ofisi yake. Rais Macron hataki kupoteza muda kabla ya wiki muhimu ya kwanza katika miaka yake mitano ya uongozi.

Emmanuel Macron anatarajiwa kumteua waziri wake mkuu.
Emmanuel Macron anatarajiwa kumteua waziri wake mkuu. CHARLY TRIBALLEAU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Saa chache baada ya kukabidhiwa madara na mtangulizi wake François Hollande, rais Emmanuel Macron amesema hataki kupoteza muda. Hata kabla ya kukabidhiwa madaraka siku ya Jumapili, washirika wake wa karibu walitangaza majina ya sehemu ya kwanza ya maafisa wa ofisi yake. Ishara ya nia yake ya kuendeleza uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani, Emmanuel Macron alimteua kama mshauri katika masuala ya kidiplomasia balozi wa sasa Ufaransa nchini Ujerumani, Philippe Etienne, mwenye umri wa miaka 61. Bw Etienne, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Alain Juppe kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka1997 na katika utawala wa Nicolas Sarkozy kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2010. Alikuwa mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Ulaya mjini Brussels kuanzia mwaka 2007 hadi 2010.

Mkuu wa zamani wa ofisi yake mjini Bercy, Alexis Kohler, mwenye umri wa miaka 44, aliteuliwa katibu mkuu wa Elysee. Patrick Strzoda, kwa upande wake, ameteuliwa mkuu wa ofisi ya rais Emmanuel macron, wakati ambapo Ismael Emelien ameteuliwa mshauri maalum wa Emmanuel Macron.

Emmanuel Macron, tayari kushinikizwa

Jumatatu Mei 15, Emmanuel Macron ataanza wiki muhimu ya kwanza katika uongozi wake wa miaka 5. Rais Emmanuel Macron anatarajiwa kutangaza jina la Waziri Mkuu. Uchaguzi ambao ni muhimu katika mchezo wa ushirikiano anaotafuta kwa uchaguzi wa wabunge na kwa muhula wake wa miaka mitano.

Kwa sasa, Edouard Philippe, Meya wa LR mjini Havre ni mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kushikilia wadhifa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.