Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-TRUMP

Fuata moja kwa moja kuapishwa kwa Donald Trump

Donald Trump anaapishwa leo Ijumaa, Januari 20 kama rais 45 wa Marekani. Ataapishwa kwenye ukumbi wa Capitol Hill saa 05:46 saa za Washington (sawa na 01:46 jioni saa za Afrika ya Mashariki).

Donald Trump akiwasili katika ukumbi wa Capitole kwa sherehe za kuapishwa,Januari 20, 2017.
Donald Trump akiwasili katika ukumbi wa Capitole kwa sherehe za kuapishwa,Januari 20, 2017. SAUL LOEB / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

19:33 Rais mteule Donald Trump na mkewe Melanie wako katika eneo atapoapishwa Trump.

19:14 Rais Obama na mwenzake mteule Trump wameondoka katika ikulu ya White House pamoja na sasa wako katika eneo atakaloapishwa Trump.

19:00 Waandamanaji waliovalia nguo nyeusi wametupa mapipa ya taka barabarani na kuvunja vioo vya madirisha ya maduka. 

Walinzi walifunga eneo moja la kuingilia baada ya kuvamiwa na waandamanaji wa Black Lives Matter. 

Waandamanaji waliimba nyimbo dhidi ya Trump na kuwazuia watu kuingia katika eneo hilo la kuapihswa kwa Trump.

Lakini wafuasi wa Trump waliwapigia kelele waandamanaji hao. Wakati huohuo makamu wa rais wa zamani nchini Marekani akiwemo Dan Quayle naDick Cheney wamefika na kuketi.

 Mkewe Obama na Melanie Trump pia wako katika gari mbele ya viongozi hao wakielekea Capitol Hill.  

Makamu wa rais Joe Bidden na makamu wa rais mteule Mike Pence wamewasili katika eneo ambako Trump Ataapishwa
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.