Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

MLC yarudi kwenye meza ya mazungumzo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mazungumzo ya kisiasa yameendelea Jumatano hii, huku chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba na washirika wake ambao walikatisha kushiriki kwao katika mazungumzo ya kitaifa wakirudi kwenye meza ya mazungumzo.

Makao makuu ya chama cha MLC cha  Jean-Pierre Bemba nchini DRC.
Makao makuu ya chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba nchini DRC. RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Muungano huu wa vyama vya upinzani wa FRC ulisema Jumanne wiki hii kwamba unajiondoa kwenye mazungumzo.

Muungano huu unabaini kwamba unawakilishwa katika mazungumzo hayo.

Lakini mashauriano yanaendelea ili kuwashawishi kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

FRC ni muungano unaoundwa na chama cha MLC, vyama zaidi ya arobaini na mashirika ya kiraia hamsini.

Mazungumzo haya yanafanyika ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kumalizika kwa muhula wa Rais Joseph Kabila, ambao unamalizika tarehe 20 Desemba.

Kurefushwa kwa muda wa kalenda ya uchaguzi imezua mgogoro wa kisiasa nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.