Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Ali Bongo ataka kufanya marekebisho

Ali Bongo Ondimba aliyechaguliwa kwa muhula wa pili, ameelezea wito wake kwa ajili ya mazungumzo na upinzani. Mazungumzo ambayo yatafanyika kwa kutafakari suala lamageuzi ya kitaasisi na kikatiba.

Ali Bongo Ondimba wakati akihojiwa na vyombo vya habari mjini Libreville, nchini Gabon, Septemba 24, 2016.
Ali Bongo Ondimba wakati akihojiwa na vyombo vya habari mjini Libreville, nchini Gabon, Septemba 24, 2016. REUTERS/Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mapendekezo haya ya mageuzi, kuna suala la kuchaguliwa kwa duru mbili au kusitisha mihula na muda wa mihula kwa kuliongoza taifa. Lakini maelewano haya yatapatikana bila ya ushiriki wa jumuiya ya kimataifa, amesisitiza Waziri wa Mawasiliano na Msemaji wa serikali ya Gabon, Alain-Claude Bacille By Nze.

Akizungumza na Deusch Welle, Alain-Claude Bacile By Nze amesema, upinzani, ambao bado unapinga kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Ali Bongo Ondimba, wanaamini kuwa kipaumbele kipo mahali pengine.

Bw Bacile By Nze amewataka wanasiasa wa Gabon kuwa kitu kimoja na kuweka kando tufauti zao kwa kulijenga taifa. Amesema rais Ali Bongo ana nia njema ya kuwaleta pamoja wanasiasa kwa ujenzi wa taifa la Gabon.

Wakati huo huo Rais Ali Bongo amemteua Emmanuel Issoze-Ngondet kuwa Waziri Mkuu akimtaka kuharakia kuunda "Serikali ya umoja"

Emmanuel Issoze-Ngondet alikua bado akihudumu kama Waziri wa mambo ya Nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.