Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Makubaliano ya amani kutiwa saini, siku ya kihistoria Colombia

Colombia inajiandaa kuingia katika ukurasa mpya wa kihistoria, Jumatatu hii, Septemba 26, 2016, pamoja na sherehe ya kutia saini mkataba wa amani kati ya serikali na waasi wa kundi la FARC katika mji wa Cartagena.

Ivan Marquez, mjumbe wa FARC katika mazungumzo (kushoto) akimsabahi kwa mkono Humberto de la Calle (kulia) wakati wa mkataba wa amani wa kihistoria nchni  Colombia ulioafikiwa mjini Havana, Agosti 24, 2016.
Ivan Marquez, mjumbe wa FARC katika mazungumzo (kushoto) akimsabahi kwa mkono Humberto de la Calle (kulia) wakati wa mkataba wa amani wa kihistoria nchni Colombia ulioafikiwa mjini Havana, Agosti 24, 2016. REUTERS/Alexandre Meneghini
Matangazo ya kibiashara

Watu 2,500 wamealikwa kusherehekea wakati huu wa kihistoria ambao unatamatisha zaidi ya miaka 50 ya vita na kundi kubwa la watu wenye silaha katika bara la Amerika. Mgogoro ambao amesababidha vifo vya watu 220 000, huku watu 40,000 wakitoweka na wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 7 nchini kote.

Ilibidi miaka minne ya mazungumzo kati ya serikali na waasi wa kundi la FARC ili kuhitimisha makubaliano hayo. Mikataba ambayo haiungwi mkono kwa kauli moja, wapinzani wanakosoa ahadi za serikali kwa waasi na dhamana haitoshi. "Bora amani isio kamili kuliko vita kamili," amejibu Rais wa Colombia Juan Manuel Santos.

Siku ya Ijumaa, kundi la waasi la FARC lilitangaza kuridhia mikataba isiyopingwa, katika mkutano wake wa kumi. "Vita vimemalizika," amesema kiongozi wa ujumbe wa kundi la waasi la FARC katika mazungumzo Ivan Marquez.

Mikataba ilisainiwa katika mji wa Havana Agosti 24 kati ya pande mbili zilizokua zikishiriki mazungumzo. Lakini kulikua kunahitajika tendo la kihistoria kwenye ardhi ya Colombia ili kuidhinisha makubaliano hayo.

Marais kumi na tano kutoa nchi mbalimbali, Mawaziri wa Mambo ya Nje na viongozi wa ngazi za juu, ikiwa ni pamoja na Rais wa Cuba Raul Castro,mwenyeji wa mazungumzo ya amani, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, wanahudhuria sherehe hizo. Mikataba hiyo inatazamiwa kusainiwa saa 11 jioni saa za Colombia(sawa na saa 4:00 usiku saa za kimataifa ) Jumatatu hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.