Pata taarifa kuu
KENYA-CORD-SIASA

CORD mbioni kuanzisha mchakato wa kuwatafuta viongozi wake wapya

Muungano wa kisiasa wa CORD nchini Kenya, kupitia vyama vyao umetangaza kuanza mchakato wa kuziba nafasi ya viongozi wa vyama vyao na wabunge kutoka kwenye muungano huo, ambao wametangaza kujiunga na chama kipya cha Jubilee.

Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama
Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu, vyama vya upinzani vinavyounda muungano wa CORD vimeshuhudia baadhi ya wanachama wake mashuhuri wakitangaza kuhama vyama vyao na kwenda kujiunga na chama tawala wa Jubilee ambacho kiliundwa mwishoni mwa juma lililopita.

Akizungumza kwenye makao makuu ya chama cha FORD Kenya, kinara wa chama hicho Moses Wetang’ula, amesema chama chake kimeanza kuziba nafasi za wabunge wa pwani na wengine waliotangaza kwenda Jubilee, huku akiitaka tume ya uchaguzi IEBC kujiandaa na chaguzi ndogo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya ODM, nacho pia hakikuachwa nyuma, ambapo wabunge wake kadhaa kutoka maeneo ya pwani, wameanza kampeni kupigia debe chama kipya cha Jubilee, wakikaidi tishio la kufutwa ndani ya chama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.