Pata taarifa kuu
-SIASA

Gabon: Ali Bongo achaguliwa kuwa rais, upinzani wapinga

Ali Bongo amechaguliwa tena kwa muhula wa pili kuwa rais wa Gabon kwa 49.80% ya kura, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Kiwango cha ushiriki kilifikia 59.46%. Upinzani umepinga matokeo hayo yaliyotangazwa na Wizara ya mambo ya Ndani, ukubaini kwamba kura za mgombea wao ziliibwa.

Vikosi vya usalamakatika mji wa Libreville vikitumia mizinga ya maji dhidi ya waandamanaji, Agosti 31, 2016.
Vikosi vya usalamakatika mji wa Libreville vikitumia mizinga ya maji dhidi ya waandamanaji, Agosti 31, 2016. AFP/Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Jean Ping, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, ambaye leo mwanasiasa wa upinzani, ameshutumu matokeo hayo. Amesema kura zake ziliibwa hasa katika mkoa wa Haut-Ogooué, mkoa inakoishi familia Bongo na kwa mujibu wa takwimu rasmi, Ali Bongo ameshinda kwa zaidi ya 95% ya kura. kiwango cha ushiriki, kilifikia karibu 100%.

Kwa upande wa mmoja wa wawakilishi wa upinzani katika Tume Huru ya Uchaguzi, ambaye amejiuzulu muda si mrefu kwenye Tume hiyo, amesema matokeo hayo hayaendani na kura walizokua wamehesabu, akibaini kwamba ni kashfa kwa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Gabon. Mjumbe huyo amekataa kusahihisha takwimu hizo. Mbali na hilo, kwa jumla ya wajumbe wanane wa Tume Huru ya Uchaguzi (Cenap), wanne pekee ndio wamekubalisha matokeo yaliyotangazwa saa moja iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mara baada ya tangazo la waziri wa Mambo ya Ndani, wafuasi wa upinzani wameingia mitaani kukemea kile walichokiita udanganyifu na kupiga kelele "Ali Bongo anapaswa kuondoka". Katika mji wa Libreville, vikosi vya usalama vimetumia mabomu ya machozi kwa kuwazuia waandamanaji wasikurubiimajengo ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Makabiliano yametokea katika mji wa Libreville kati ya wafuasi wa Ali Bongo Ondimba aliyechaguliwa tena kuwa rais, na wale wa Jean Ping, mgombea wa katika uchaguzi ambaye amechukua nafasi ya pili Agosti 31, 2016.
Makabiliano yametokea katika mji wa Libreville kati ya wafuasi wa Ali Bongo Ondimba aliyechaguliwa tena kuwa rais, na wale wa Jean Ping, mgombea wa katika uchaguzi ambaye amechukua nafasi ya pili Agosti 31, 2016. AFP/Marco Longari

Mikusanyiko ya watu pia imeshuhudiwa katika mji wa Port-Gentil, mji wa pili nchini Gabon, wenye wafuasi wengi kutoka kambi ya upinzani. Kwa mujibu wa mkazi mmoja wa mji huo, wapinzani walitawanywa na mizinga ya maji.

Waziri wa Mambo ya Ndani aametangaza matokeo yaliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi (Cenap). Ali Bongo amechaguliwa tena kwa 49.80% ya kura. Mpinzani wake Jean Ping amepata 48.23% ya kura. kiwango cha ushiriki kilifikia 59.46%.

Kabla ya matangazo hayo ya mwisho, Jumuiya ya Kimataifa ilitoa shinikizo kwa serikali na Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya mwisho.

Kikatiba, matokeo ya mwisho yalistahili kutangazwa siku ya Jumanne, ucheleweshwaji ambao ulizua hali ya wasiwasi.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya katika ripoti hiyo ya awali walisema kuwa, Uchaguzi huo haukuwa wazi.

Mwaka 2009 vurugu zilizuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.